Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Margaret Vogt afariki dunia, Ban asema UM utamkumbuka kwa utendaji wake

UN Photo/JC McIlwaine
Margaret Vogt enzi za uhai wake. Hapa alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini New York. (Picha:

Margaret Vogt afariki dunia, Ban asema UM utamkumbuka kwa utendaji wake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza masikitiko yake kufuatia taarifa za kifo cha Margaret Vogt ambaye alikuwa mwakilishi wake maalum huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kuanzia mwaka 2011 to 2013.

Kifo chake kimetokea Jumatano ya Septemba 24 ambapo Katibu Mkuu amesema mchango wake ndani ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika na hata kitaaluma ulikuwa ni wa kipekee.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Ban akimwelekezea marehemu Vogt kuwa alikuwa ni mtu alitambulika kwa kazi yake aliyofanya bila kuchoka, bila kusahau wema wake na ujasiri aliioonyesha wakati akitekeleza majukumu kwenye maeneo hatarishi.

Katibu mkuu pamoja na kutuma rambirambi kwa familia ya marehemu, amesifu uongozi wa Vogt enzi za uhai wake ikiwemo wakati wa mzozo huko Somalia na CAR akisema aliokoa maisha ya wengi, alikuwa mfano kwa wengine na hata kuleta furaha kwa wale aliokutana nao na aliofanya nao kazi.

Ban amesema marafiki wengi walivutiwa na utendaji wake na kwamba Umoja wa Mataifa utamkumbuka kwa utu wake.