Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malkia Letizia wa Hispania ashiriki katika mapambano dhidi ya njaa na utapiamlo

Malkia Letizia wa Hispania ashiriki katika mapambano dhidi ya njaa na utapiamlo

Mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva na Malkia Letizia wa Hispania.[Picha©FAO/Paulo Caruso Dias De Lima[/caption]Malkia Letizia wa Hispania ni miongoni mwa viongozi waliothibitisha kushiriki na kuhutubia  katika mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu lishe utakaofanyika katika makao makuu ya shirika la chakula na kilimo FAO  mjini Rome Italia.

Taarifa ya FAO kwa vyombo vya habari inasema kuwa malkia Letizia ataungana na jumuiya ya kimataifa katika juhudi za kupambana na njaa na utapiamlo na kwamba amethibitisha hilo  baada ya kukutana na Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva kandoni mwa mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo imemkariri mkuu wa FAO José Graziano da Silva akishukuru Hispania kwa mchango wake katika kupambana na njaa na utapiamlo hususani ukanda wa Amerika ya Kati.

Viongozi  hao waliyakita mazungumzo yao katika umuhimu wa kuimarisha mlo na kukuza kiwango cha lishe huku wakisikitishwa na kukuwa ghafla kwa kiwango cha utipwatipwa kwa watoto na kwa watu wazima.

Kwa mujibu wa FAO watu bilioni mbili dunini wana upungufu wa aina moja au zaidi wa virutubisho huku watu zaidi ya bilioni moja wakiwa na uzito uliokithiri ambapo watu milioni 500 wana ugonjwa wa utipwatipwa