Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika imeanza kuibuka baada ya ukoloni mamboleo: Museveni

UN Photo/Kim Haughton
Rais Yoweri Museveni wa Uganda.Picha ya

Afrika imeanza kuibuka baada ya ukoloni mamboleo: Museveni

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amehutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akiangazia masuala kadhaa ikiwemo chanzo cha mizozo na migongano inayotoea sasa barani Afrika na marekebisho ya vyombo vya Umoja wa Mataifa.

Mathalani kuhusu marekebisho amesema ni vyema vyombo hivyo vikaakisi hali halisi ya ulimwengu wa sasa na hivyo Uganda itashikia kasi suala hilo. Kuhusu mwelekeo wa Afrika Rais Museveni amesema baada ya miaka zaidi ya 500 ya utumwa, ukoloni na ukoloni mamboleo, Afrika sasa inaibukia kwenye mwanga.

Baada ya kutoa hotuba yake, Rais Museveni alimweleza mwandishi wetu kwa muhtasari kile alichoangazia.

(Sauti ya Museveni)