Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa kupanua matumizi ya kiwango cha chini cha kaboni na nishati mbadala wazinduliwa

UN Photo/Eskinder Debebe)
UN Photo/Eskinder Debebe

Mpango wa kupanua matumizi ya kiwango cha chini cha kaboni na nishati mbadala wazinduliwa

Viongozi wa serikali na makundi yasiyo ya kiserikali wametangaza mipango miwili ya kupanua upatikanaji wa nishati safi mbadala maradufu kwa watu katika mashariki na kusini mwa Afrika na mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea.

Mpango huo wa nishati safi Afrika una lengo la kupanua sehemu ya nishati mbadala inayotumiwa na mataifa ya Afrika Mashariki na Kusini kutoka kwa kiwango cha sasa cha asilimia 12 hadi angalau asilimia 40 ifikapo mwaka 2030.

Mpango wa upanuzi wa umeme wa mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea utaimarisha ushirikiano wa kimataifa na kasi ya maendeleo ya vyanzo mbadala vya viwango vya chini vya kaboni/mkaa, kwa lengo la kufunga megawati zipatazo 120 za nishati mbadala katika nchi hizi kufikia mwaka wa 2019.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema amefurahishwa kuona mipango ambayo itapanua usambazaji wa nishati safi, nishati mbadala kwa watu Mashariki na Kusini mwa Afrika na mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea, na kuongezea kuwa, mipango hiyo itasaidia kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na kuchangia kuboresha afya, utajiri na nafasi, na maisha ya heshima kwa wote.