Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampuni za nishati kushirikiana kupunguza uchafuzi wa hewa wa muda mfupi

UN Photo.
Kwa kuimarisha nguvu ya jua, Falme za Kiarabu ni kukata uzalishaji wa gesi chafuzi, kuzalisha ajira na kuweka msingi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi chini ya kaboni. Picha:

Kampuni za nishati kushirikiana kupunguza uchafuzi wa hewa wa muda mfupi

Kampuni za kimataifa za mafuta na gesi zimejiunga na serikali na mashirika ya kimataifa ya mazingira katika kupunguza uzalishaji wa gesi sugu ya methane, inayozalishwa  na sekta ya mafuta na gesi, kama sehemu ya ubia wa sekta ya mafuta na gesi ya methane.

Mpango huo ulizinduliwa leo katika Mkutano wa Tabianchi, chini ya Ushirikiano wa Hewa Safi wa  kupunguza  vichafuzi vya hewa vya muda mfupi.

Tangazo hilo ni mojawapo ya matangazo matano yaliyotolewa leo na viongozi wa sekta ya viwanda, serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali,  ya kusaidia kupunguza uzalishaji wa muda mfupi wa vichafuzi vya mazingira na ufumbuzi wa masuluhu ya hali ya hewa kutoka sekta kadhaa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amefurahi kuona mipango mathubuti ya kusaidia kupunguza kutolewa kwa vichafuzi vya mazingira vya muda mfupi angani.

Halikadhalika, Ban amesema matangazo haya yanaonyesha jinsi serikali, mashirika na asasi za kiraia zinaweza kufanya kazi pamoja kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi.