Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Inachodai Afrika juu ya mabadiliko ya tabianchi ni stahili yake: Kikwete

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihutubia mkutano wa mazingira kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York. (Picha:UN /Cia Pak)

Inachodai Afrika juu ya mabadiliko ya tabianchi ni stahili yake: Kikwete

Mkutano wa viongozi wa dunia kuhusu mazingira umefikia ukomo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huku bara la Afrika likitaka kuungwa mkono kwenye hatua ambazo tayari inachukua kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Sauti ya Afrika iliwasilishwa na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakati mkutano huo ulipofanya hitimisho la kusikiliza matamko yenye utashi wa kisiasa kutoka kwa viongozi ambapo katika mahojiano maalum na Idhaa hii baada ya mkutano huo amesema tayari Afrika imeanza kuchukua hatua kwa hiyo…..

(Sauti ya Rais Kikwete)

Rais Kikwete akatolea mfano wa matumizi ya mkaa na msaada ambao ambao Afrika inahitaji.

(Sauti ya Rais Kikwete)

Mahojiano kamili na Rais Kikwete yatapatikana kwenye ukurasa wetu.