Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuchukua hatua kuhusu tabianchi kutaleta faida nyingi- Kutesa

UN Photo/Devra Berkowitz
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Sam Kutesa,(

Kuchukua hatua kuhusu tabianchi kutaleta faida nyingi- Kutesa

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Sam Kutesa, ameziambia nchi wanachama kuwa mabadiliko ya tabianchi ni suala la dharura, na lenye uwezekano wa kuhatarisha maisha, kudhoofisha fursa za maendeleo na juhudi za kutokomeza umaskini na kufikia maendeleo endelevu.

Bwana Kutesa amesema hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa viongozi wa dunia kuhusu tabianchi, ambao unafanyika mjini New York leo Jumanne tarehe 23, ambako amesisitiza malengo ya mkutano huo:

“Tunakusanyika hapa na dhamira mbili: kuchagiza utashi wa kisiasa ili kukamilisha mkataba yakinifu wa mabadiliko ya tabianchi mjini Paris Disemba 2015, na kuibua hatua mathubuti za kuongeza uhimili na kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na kuuelekeza ulimwengu kwenye uchumi unaojali mazingira.”

Rais huyo wa Baraza Kuu amesema kuna faida kubwa inayoweza kutokana na kuchukua hatua kuhusu tabianchi, akisema kuchukua hatua kunaweza  kuongeza na pia kulinda ufanisi wa maendeleo. Ameongeza kuwa kutaongeza nafasi za uwekezaji, fursa za ajira na ukuaji wa uchumi.