Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wekeni historia, au historia iwaponde: DiCaprio awaeleza wakuu wan chi

Wekeni historia, au historia iwaponde: DiCaprio awaeleza wakuu wan chi

Mjumbe wa amani wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya tabianchi, Leonardo DiCaprio amesema mkutano wa mwaka huu wa wakuu wa nchi kuhusu mabadiliko ya tabianchi ni jumuiko linalotakiwa kuchukua uamuzi jasiri zaidi ya yale anayotakiwa kufanya mtu binafsi.

Akiwahutubia wakuu hao kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, DiCaprio ambaye ni mcheza filamu mashuhuri amesema...

(Sauti ya DiCaprio)

"Marafiki zangu, chombo hiki, pengine kuliko mkusanyiko wowote ule katika historia ya binadamu, sasa hivi kinakabiliwa na jukumu hili gumu ambalo pia linaweza kutekelezeka .Mnaweza kuweka historia au historia inaweza kuwaponda. Kusema wazi janga hili ni zaidi ya uamuzi anaopaswa kufanya mtu mmoja mmoja. Hii inahusu viwanda vyetu na serikali zetu dunia kuchukua uamuzi mkubwa wa vitendo.”

DiCaprio amesema sasa ni wakati wa vitendo na maandamano yaliyoshuhudiwa Jumapili duniani kote kutaka serikali kuchukua hatua za dhati ni mwanzo tu wa hatua za binadamu kuona sayari ya dunia inalindwa.