Ukanda wa maziwa makuu wakubaliana kuhusu mustakhbali wa FDLR

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe(kushoto) akihojiwa na Assumpta Massoi wa Radio ya UM. (Picha:UN/Joseph Msami)

Ukanda wa maziwa makuu wakubaliana kuhusu mustakhbali wa FDLR

Mkutano wa nne kuhusu mpango wa amani, usalama na ushirikiano huko Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, DRC uliomalizika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjiniNew York, umeafikiana mambo makuu matatu kuhusu kikundi cha waasi cha FDLR nchini DR Congo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Benard Membe ambaye alihudhuria kikao hicho akimwakilisha rais Jakaya Kikwete, ametaja mambo hayo kuwa ni Mosi, FDLR kuzingatia muda wa miezi sita waliopatiwa kujisalimisha kwa mujibu wa makubaliano ya Angola, Pili, wadau ikiwemo Umoja wa Mataifa washirikiane na FDLR kuhakikisha wanatekeleza suala lao la kujisalimisha na kwamba …

(Sauti ya Membe)

Membe pia akatolea ufafanuzi suala laKisanganiambako FDLR wanatakiwa kujisalimishia.

(Sauti ya Membe)

Mpango wa makubaliano ya amani, usalama na ushirikiano ulisainiwa Februari, mwaka 2013 huko Addis Ababa na nchi 11 za ukanda wa maziwa makuu.