Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muungano wa nchi za Kiarabu wachukua hatua kutetea haki za watoto vitani

Muungano wa nchi za Kiarabu wachukua hatua kutetea haki za watoto vitani

Muungano wa nchi za Kiarabu na Ofisi ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu watoto katika mizozo ya silaha, wamefanya makubaliano leo ya kuimarisha ulinzi wa watoto wanaoathiriwa na mizozo ya silaha katika nchi za Kiarabu.

Ushirikiano huo ulitiwa saini na Dkt. Nabil Elaraby, Katibu Mkuu wa Muungano wa Nchi za Kiarabu na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson.

Dkt. Elaraby amesema anatumai kuwa makubaliano hayo yatakuwa hatua muhimu katika kuhakikisha watoto wanalindwa, na kutimiza lengo la pamoja la kuwa na nchi za Kiarabu ambapo watoto watakua katika mazingira ya amani.

Nchi za Kiarabu zimeshuhudia mabadiliko mengi ya kisiasa na kijamii katika nyakati za hivi karibuni, na ulinzi wa uhai na haki za watoto ni suala la kipaumbele.