Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasichana, wanawake tuanze kuleta mabadiliko: Nancy awaeleza wake wa Rais

UN Photo/Amanda Voisard
Nancy Tomee akihutubia wake wa Marais wa Afrika na wageni waalikwa kwenye moja ya kumbi za UM mjini New York. (Picha:

Wasichana, wanawake tuanze kuleta mabadiliko: Nancy awaeleza wake wa Rais

Wake wa Rais wa Afrika waliokutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kujadili mustakhbali wa afya ya mama na mtoto barani humo, wameombwa washiriki kikamilifu katika kuunga mkono harakati za ulinzi wa afya ya mama na mtoto, wakati huu ambapo mtoto wa kike barani Afrika anakumbwa na madhila lukuki ikiwemo mila potofu. Wito huo ulielekezwa kwao na Nancy Tomee, wa jamii ya Pokot nchiniKenyaambaye alikataa kukeketwa na sasa amesimama kidete kutetea kutokomezwa kwa mila hiyo potofu. Akihutubia kwa Kiswahili,Nancyamesema sasa ni wakati wa mabadiliko, na mabadiliko hayo yaanzie kwa wasichana na wanawake wenyewe. Fuatana naye katika hotuba hii.