Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia kuthibitisha ahadi zao za kutoa kipaumbele kwa watu katika maendeleo

Umoja wa Mataifa.Picha ya UM

Viongozi wa dunia kuthibitisha ahadi zao za kutoa kipaumbele kwa watu katika maendeleo

Kikao Maalum cha viongozi wa dunia kitafanyika kwenye Umoja wa Mataifa tarehe 22 Septemba kutathmini hatua zilizochukuliwa na serikali katika kipindi cha miaka 20 za kuboresha maisha ya watu na masuala ya idadi ya watu

Wakuu wa nchi na wawakilishi wengine wa Serikali watakusanyika kwenye Kikao hicho Maalum cha kuadhimisha miaka 20 ya Mkutano wa Kimataifa wa Idadi ya Watu na Maendeleo uliofanyika mjini Cairo mwaka 1994, na kuthibitisha ahadi zao na kuweka watu msitari wa mbele katika maendeleo.

Mkutano wa Cairo ulikuwa wakati muhimu katika historia ya mjadala kuhusu uhusiano kati ya idadi ya watu na maendeleo.

Mkutano huo uliafikia makubaliano ya aina yake kati ya nchi wanachama 179 wa Umoja wa Mataifa ya kuwa haki na ustawi wa watu binafsi ni lazima liwe lengo kuu katika juhudi za kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mkutano huo ulitoa Mpango wa Utekelezaji uliosisitiza umuhimu wa kulinda haki za binadamu, hasa haki za wanawake na vijana, kuwekeza katika afya na elimu, kuendeleza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake, pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya na haki za uzazi.

Halikadhalika, hatua hizo zilionekana kama fursa muhimu ya kupanua haki kwa wote na muhimu kwa ajili ya maendeleo endelevu