Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chapisho kuhusu adhabu ya Kifo kuzinduliwa wakati wa kikao cha Baraza Kuu

Gereza.Picha ya UM/Martine Perret

Chapisho kuhusu adhabu ya Kifo kuzinduliwa wakati wa kikao cha Baraza Kuu

Tarehe 25 mwezi huu wa Septemba, Ofisi ya haki za binadamu ya  Umoja wa Mataifa itazindua chapicho kuhusu adhabu ya Kifo. Tukio hilo litafanyika wakati ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa unapigia chepuo kutokomezwa kwa adhabu hiyo. Maazimio kadhaa yamepitishwa kutaka nchi zinazotekeleza adhabu hiyo zisitishe mara moja kwani adhabu hiyo ni kinyume na haki za binadamu. Tangu mwaka 2007 Baraza Kuu limeridhia maazimio matatu ya kutaka nchi wanachama kusitisha adhabu hiyo na hatimaye kutokomeza huku Kamati ya tatu ya baraza hilo mwaka 2012 ikipitisha kwa kishindo azimio kuhusu sualahilo. Je nchini Tanzaniaambako adhabu ya kifo bado inatambulika kisheria hali ikoje? Basi ungana na Assumpta Massoi katika makala hii.