Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ni sasa:WMO

Wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ni sasa:WMO

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuanzia September 23 mwaka huu. Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva Katibu Mkuu wa WMO Michel Jarraud amesema kuna udharura wa kupunguza gesi chafuzi kwa kuzingatia ushihidi wa kisayansi kuwa zinaharibu mazingira .

Amesema mkutano huo na juhudi ambazo zimeshachukuliwa katika makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi unasisitiza umuhimu wa hatua za jumuiya ya kimataifa kuzidi kuchukua hatua haraka akisema mabadiliko hayo yanaweza kuongeza joto na usawa wa bahari ambao ni hatari kwa karne zijazo..

Bwana Jarraud amesema mabadiiko ya tabia nchi yanapunguza acid ya baharini na kutishia uhai wa bahari. Amesema ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa nisawa na kukopa fedha kwa watoto na kuwaachia mzigo mkubwa wa deni.