Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Manusura wamahiaji wasema walilazimishwa kuhama mashua

Manusura wa ajali ya boti kisiwa cha Lampedusa (Picha ya maktaba/UNHCR)

Manusura wamahiaji wasema walilazimishwa kuhama mashua

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema manusura wa ajali katika bahari ya Mediterranean wamesema walilazimishwa kubadilisha chombo cha usafiri mara tatu na pale walipokataa kuhamia katika mashua ndogo kwasababu za kiusalama walitishiwa kuwa wangerudishwa Misri

Kwa mujibu wa taarifa ya IOM mashuhuda wanne miongoni mwa sita ambao ni wahamaji walisisitiza kurudishwa kuliko kuhamia katika mashua ndogo na ndipo wasafirishaji hao haramu ambao wanadaiwa ni kutoka Palestina na Misri walipoanza kuwachapa bakora na kuwakemea.

Wamesema kuwa mashua ya maharamia ilisogelea ile waliyokuwamo wahamiaji ambayo baadhi yao walikuwa wamehamia katika mashua ndogo. Manusura wanasema waliwalazimishwa kuingia majini na kisha wakaizamisha mashua ndogo kwa kutumia yao kubwa. Katika ushuhuda wao wamesema wauaji hao walikaaa sehemu hadi walipojiridhisha kuwa chombo hiko kimezama.

“Baada ya kukipiga chombo chetu walisubiri kuhakikisha imezama kabisa kabla ya kuondoka . Walikuwa wanacheka ” amesema mmoja wa manusura na kuongeza kuwa watu hao waliwakejehi kwa vicheko.

Ameongeza kuwa mashua ilipopigwa kwa mara ya kwanza mmoja wa abiria alijiua kwa kukata tamaa. IOM inasema kuwa wahamiaji zaidi ya 400 walikuwemo katika mashua hiyo huku ikiaminika kuwa zaidi ya watoto 100 wameakufa maji.