Ban akaribisha ubadilishanaji mamlaka kutoka MISCA kuwa MINUSCA huko CAR
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha kuanza kwa mamlaka mpya ya ulinzi ya Umoja huo ya kulinda amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA kutoka ile ya awali ya Muungano wa Afrika, MISCA.
Kubadilishana huko kwa mamlaka kumefanyika baada ya kukamilika kwa muda wa MISCA na hivyo kuashiria mwanzo wa hatua ya kijeshi na polisi ya MINUSCA huko CAR.
MINUSCA ina wanajeshi 6500, polisi 1000 na kundi la watendaji wa kiraia na wanaendelea kusambazwa maeneo mbali mbali ya nchi hiyo na lengo kuu ni kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na kusaidia mchakato wa kisiasa na ujenzi wa nchi.
Katibu Mkuu ameshukuru MISCA na vikosi vya Ufaransa kwa kulinda maisha ya watu wengi.
Halikadhalika ameshukuru ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika pamoja na kuhakikisha makabidhiano muafaka wa mamalaka, kwa mujibu wa viwango Umoja wa Mataifa.