Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres na Angelina Jolie waonya kuhusu tatizo la ajali za boti Mediterenia

Mjumbe Maalum kuhusu wakimbizi, Angelina Jolie akutana na mkimbizi kutoka Syria akiwa ziarani Aleppo ambaye alipoteza mkewe na msichana wake wakati boti lao.© UNHCR/P.Muller

Guterres na Angelina Jolie waonya kuhusu tatizo la ajali za boti Mediterenia

Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, António Guterres na Mjumbe Maalum kuhusu wakimbizi, Angelina Jolie, wameonya kuwa tatizo la ajali za watu kuzama kwenye Bahari ya Mediterenia wanapojaribu kuvuka kwenda ulaya linaendelea kuwa sugu.

Guterres na Jolie wamesema hayo baada ya kuzuru makao ya wanajeshi wa Malta wanaohusika na uokozi wa majini hapo jana, wakati habari za boti nyingine kuzama Misri na Libya zikiripotiwa na kuwaua watu zaidi.

Bwana Guterres na Bi Jolie walikutana na manusura watatu wa ajali moja ya boti, ambao walikuwa wamenusuriwa na chombo cha kusafirisha shehena na kupelekwa Malta.

Akiwa kwenye mji mkuu wa Malta, Valletta, Bi Jolie pia alitembelea familia za wakimbizi wa Syria ambao walinusurika ajali mbaya mwezi Oktoba mwaka 2013. Nusu ya watu wanaowasili barani Ulaya kwa boti ni wakimbizi kutoka Syria na Eritrea. Zaidi ya watu 2,500 wamezama au kutoweka wakati wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterenia mwaka huu pekee, wakiwemo 2,200 kutoka mwanzoni mwa mwezi Juni.