Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ibn Chambas ahutubia Baraza la AU la Amani na usalama kuhusu Darfur

UN Photo/Paulo Filgueiras
Mohamed Ibn Chambas, Mwakilishi wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika. Picha:

Ibn Chambas ahutubia Baraza la AU la Amani na usalama kuhusu Darfur

Mwakilishi maalum wa Pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa na mptanishi kuhusu Darfur, Ibn amelihutubia Baraza la Amani na Usalama la AU mjini Addis Ababa na kuelezea juhudi za upatanishi alizoanzisha kwa ushirikiano na jopo la utekelezaji la AU na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Sudan na Sudan Kusini, pamoja na IGAD.

Katika hotuba yake, Chambas ameangazia njia za kutumia fursa iliyopo ili kujumuisha harakati za amani Darfur katika mkakati wa mazungumzo ya kitaifa yaliyotangazwa na Omar Hassan Al-Bashir mapema mwaka huu.

Ameelezea imani ya wadau wengi kuwa vita ni lazima vikomeshwe kupitia usitishaji mapigano au mkataba wa amani wa kudumu, na pia haja ya kuleta mabadiliko jumuishi yanayotokana na matakwa ya raia wote wa Sudan, yote hayo yakifanyika kwa njia ya uwazi, uhuru na haki.