Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahusika wachache wa uhalifu wa halaiki wanakumbana na mkono wa sheria: Mtaalamu

UN Photo/Amanda Voisard
Pablo De Greiff,

Wahusika wachache wa uhalifu wa halaiki wanakumbana na mkono wa sheria: Mtaalamu

Mtaalamu maalum wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za mpito Pablo de Greiff* ameonya kuwa licha ya uwajibikaji wa wazi kimataifa ni sehemu ndogo tu ya wahusika wa uhalifu wa halaiki wanaochunguzwa na kushtakiwa.

Katika taarifa yake aliyowasilisha katika baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, mtaalamu huyo amesisitiza  kuwa ni muhimu kwa mataifa kuridhia mikakati thabiti ya kuwafikisha katika sheria wahusika na kuzuia kutokea kwa matukio hayo.

Bwana Greiff amesema kuwa kwa kuweka mikakati ya mpangilio wa mashataka ya jinai,  nchi zinaweza kuongeza uwajibikaji baada ya migogoro au katika vipindi vya mpito mbali na serkali za kimabavu.

Ameshauri umuhimu wa waathirika kushiriki katika kubuni mikakati ya mashtaka na katika utekelezaji wake,  akisema kuwa ushiriki unawezesha waathirika na kuchochea uhitaji wa haki.