Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei ya vyakula yafikia kiwango cha chini zaidi katika miaka 4

Bidhaa za nafaka.Picha ya FAO

Bei ya vyakula yafikia kiwango cha chini zaidi katika miaka 4

Kipima bei za vyakula kila mwezi cha Shirika la Kilimo na Chakula, FAO, kimeonyesha kuwa bei za vyakula zilishuka mwezi Agosti kwa mwezi wa tano mfululizo na kufikia kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha miaka minne, tangu Septemba 2010.

Kipimo cha mwezi Agosti cha pointi 19.3 kilionyesha kupungua kwa pointi 7.3 tangu mwezi Julai, sawa na asilimia 3.6.

Mbali na nyama, bei za bidhaa nyingine zilishuka sana. Bei za bidhaa za ufugaji ziliongoza, zikishuka kwa asilimia 11 mwezi Agosti, na kwa asilimia 18 zikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita, kwa sababu ya uzalishaji mwingi uliofuatiwa na uagizaji mdogo kutoka ng’ambo.

Hatua ya Urusi kuzuia kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nchi kadhaa ilichangia kupunguza kwa bei za bidhaa za ufugaji. Bidhaa za nafaka pia zilishuka bei kwa asilimia 1 ikilinganishwa na mwezi Julai, na asilimia 11 ikilinganishwa na Agosti 2013. Hali nzuri ya hewa imesemekana kuchangia kuongeza uzalishaji wa nafaka kwa tani milioni 14.