Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa biashara ya hewa ya Ukaa Kenya waleta amani kwenye familia

Kitalu cha miti nchini Kenya. (Picha@WorldBank)

Mradi wa biashara ya hewa ya Ukaa Kenya waleta amani kwenye familia

Lengo namba Saba la Maendeleo ya Milenia linataka kuwepo kwa mazingira endelevu ambapo pamoja na mambo mengine nchi wanachama zinatakiwa kuwa na sera zinazozingatia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa. Kufanikisha hilo Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia chepuo biashara ya hewa ya Ukaa, yaani Carbon dioxide, ambapo wananchi wanaopanda miti wanapatiwa fedha kwani kwa kufanya hivyo miti hiyo inanyonya hewa ya Ukaa angani na kupunguza athari za hewa chafuzi. Miongoni mwa nchi zilizotekeleza mpango huo ni Kenya. Je imefanya nini? Basi ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.