OCHA yazindua tovuti mpya kuhusu baa la Sudan Kusini

10 Septemba 2014

Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA, imezindua leo tovuti mpya ya mawasiliano kuhusu Sudan Kusini yenye kichwa: janga lililoletwa na mwanadamu.

OCHA imesema kuwa, ingawa makadirio ya hivi sasa yanaonyesha kuwa njaa itashuhudiwa nchini Sudan Kusini mnamo mwaka 2015, janga lililopo sasa katika taifa hilo changa kabisa duniani limefunikwa karibuni na matatizo katika maeneo mengine duniani.

Kupitia njia ya video, picha na ramani, tovuti hiyo mpya ambayo inapatikana hapa http://southsudan.messengersofhumanity.org/ itatoa habari kuhusu maisha yalivyo sasa Sudan Kusini.

OCHA inatarajia kuwa tovuti hiyo itachagiza tena hali ya kujali kuhusu tatizo la Sudan Kusini, na kuufanya ulimwengu kuliangazia tena.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter