India yataka FAO ilinde maslahi ya wakulima wadogo

10 Septemba 2014

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva, amekuwa ziarani nchini India kuangalia jitihada za nchi hiyo kuiamrisha usalama wa chakula na kilimo endelevu ambapo ameelezwa hofu ya nchi hiyo kwa mikataba ya kimataifa ya biashara.

Katika mazungumzo yake na waziri Mkuu Narendra Modi mjini New Delhi, Da Silva ameelezwa kuwa mikataba ya aina hiyo inaweza kuathiri harakati za kuweka hakikisho la upatikanaji wa chakula na kutokomeza njaa.

Mathalani Waziri Mkuu Modi ametetea hoja ya nchi kuwa na uwezo wa kuhifadhi chakula chake cha dharura na kupigia chepuo hofu inayowakumba wakulima katika nchi maskini na zile zinazoendelea.

Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi Mkuu huyo wa FAO amesema hoja ya nchi kuwa na hifadhi ya dharura ya chakula kwani usalama wa chakula ni jambo la kwanza kabisa na sera zake zinapaswa kuzingatia mazingira ya kila nchi.

Bwana Da Silva na Waziri Mkuu Modi pia wamejadili jinsi ya kuunganisha mpango wa chakula shuleni na uzalishaji wa chakula utokanao na kilimo kwenye kaya kwa kuweka mipango ya kuwezesha ununuzi wa chakula hicho kutoka kwenye kaya za eneo husika.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter