Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza serikali mpya Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Picha ya UM(maktaba)

Ban apongeza serikali mpya Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Iraq huku akimpongeza Waziri Mkuu Hailder al- Abadi baad ya kuidhinishwa na bunge kuwa Waziir Mkuu mpya.

Katika taarifa yake Ban amesema kuwa kufikiwa kwa hatua hiyo kunafungua ukurasa mpya kwa taifa hilo hasa wakati huu kunakoshuhudia mambo ya hapa na pale. Ameongeza kusema kuwa huu ni wakati muhimu wa kuimarisha mifumo ya demokrasia ya kujenga taifa lenye utulivu na amani.

Lakini pia Ban amewatolea wito wananchi wa Iraq pamoja na makundi ya wanasiasa kushirikiana na serikali hiyo mpya ambayo imeingia mdarakani baada ya msuguano wa muda mrefu.

Amesema kuwa kwa kutambua misingi na haki za kidemokrasia Umoja wa Mataifa uko tayari kuendelea kushirikiana na serikali hiyo ambayo inaanza kufanya kazi mara moja.

Pia ametuma salama za pongezi kwa Waziri Mkuu Nuri ali-Malik ambaye amemaliza muda wake.