Daktari mwingine wa WHO kuondolewa Sierra baada ya kupatikana na Ebola

8 Septemba 2014

Daktari mwingine wa Shirika la Afya Duniani, WHO ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kituo cha matibabu ya Ebola nchini Sierra Leone amepatikana kuwa na kirusi cha Ebola baada ya vipimo. Kituo hicho cha matibabu ya Ebola kinapatikana katika hospitali ya serikali ya Kenema, ambayo inaendeshwa na Wizara ya Afya na Usafi.

WHO imesema kuwa ili kuhakikisha usalama wa wote, inapendekeza kuwa idadi ya wagonjwa wapya wanaopewa vitanda kwenye vituo vya afya ipunguzwe wakati vipimo vikiendelea kufanywa. Hali ya daktari huyo wa WHO si mbaya mno, na ataondolewa mjini Freetown muda usio mrefu.

WHO imesema kuwa wahudumu wa afya ndio uti wa mgongo wa kupambana na mlipuko wa Ebola, na kuhakikisha usalama wao ni jambo la umuhimu mkubwa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter