Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za mikoba Tanzania zawapa afueni wanawake wajawazito

UNICEF Tanzania/Pirozzi

Huduma za mikoba Tanzania zawapa afueni wanawake wajawazito

Lengo nambari tano la malengo ya maendeleo ya milenia ni kupunguza kwa asilimia 75 vifo vya wanawake wajawazito ifikapo 2015.

Tayari vifo hivyo vimepungua kwa asilimia 45 tangu 1990 duniani kote, na bado juhudi zinahitajika. Nusu ya wanawake katika nchi zinazoendelea hawapati huduma zinazofaa wakati wa ujauzito.

Ili kufanikisha lengo hili nchini Tanzania, serikali imeanza kufuatilia wanawake wajawazito hadi nyumbani kwao, katika mradi uitwao “huduma za mikoba”.

Je madaktari wanapata mafanikio? Ungana na Martin Nyoni wa radio washirika Radio SAUT ilioko Mwanza,Tanzania.