Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahalifu mwawajua hivyo chukueni hatua: Baraza la usalama laelezwa

Wahalifu mwawajua hivyo chukueni hatua: Baraza la usalama laelezwa

Msichana ambaye alikuwa mhanga wa mgogoro wa kivita huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakati akiwa na umri wa miaka 10, leo amelieleza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York kuwa ataendelea kusimulia machungu aliyopitia hadi pale hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika.

Sandra Uwiyingirimana, raia wa DRC ambaye yeye na familia yake walikimbiliaBurundina kupata hifadhi kwenye kambi ya Gatumba kuanzia mwaka 2004 amesimulia jinsi walivyovamiwa usiku wa manane na kushuhudia ukatili ikiwemo kuuawa kwa baadhi ya ndugu zake. Sandra amesema kila anaposimulia, uchungu unarejea …

(Sauti ya Sandra)

Lakini iwapo wahalifu waliokiri kushiriki kwenye mauaji yale wataendelea kutembea huru kwenye mitaa ya Burundi,  Sina chaguo, ni lazima niendelee kusimulia hadi pale jumuiya ya kimataifa itakapothibitisha kuwa maneno yangu siyo tu ya kusaka huruma bali pia kusaka uwajibikaji. Hadi pale viongozi kama ninyi na nchi mnazowakilisha mtakaponidhihirishia kuwa familia yangu na wengine wote si sawa na vitu visivyotumika tena.”

Sandra ambaye yeye na familia yake walihamia Marekani mwaka 2007 kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa wa kupatia wakimbizi makazi mapya, amesema maridhiano na amani havitapatikana iwapo hakuna haki na bila haki jinamizi la Gatumba litakuwa linarejea mara kwa mara hivyo akasema..

(Sauti ya Sandra)

“Mnazo ripoti, mnafahamu wahalifu, kutambua pekee haitoshi, ni lazime mchukue hatua.”