Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP na Bodi ya Kimataifa ya Raga Kushirikiana kupambana na Njaa kwenye Kombe la Dunia 2015

WFP RUGBY

WFP na Bodi ya Kimataifa ya Raga Kushirikiana kupambana na Njaa kwenye Kombe la Dunia 2015

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP na Bodi ya Kimataifa ya Mchezo wa Raga imezindua mpango kabambe ya kukusanyasha  fedha na kukuza uelewakamasehemu ya kupambana na njaa wakati wa komble la dunia la mchezo huo ambao utafanyika Uingereza mwakani.

Lengo la mpango huo ni kuhakikisha kabla ya kufanyika kwa michuano nambari tatu maarufu kwa ukubwa ulimwenguni ambayo itaanza September 18 mwakani, kuwepo kwa  juhudi za kuchangisha fedha katika mradi utwaoo Million Meal Challenge ya kuwasaidia wanafunzi walioko nchi zinazoendelea kupata chakula.

Ushirikiano wa Komble la Dunia  la Raga ya Kupamba na njaa umefanikiwa katika kuongeza uelewa sawa na kusaidia kazi ya WFP katika kuwalisha watu walio na njaa duniani.

Michuano hiyo itakayofanyika nchini  Uingereza inakisiwa kuwa mikubwa Zaidi kuwahi kufanyika, na mashabiki  wanazidi kuchangia katika Million Meal Challenge.

Kufikia sasa zaidi ya Dola $ 21,000 zimechangishwa kupitia kwa mchango wa hiari kupitia mauzo ya tiketi kupitia mtandao nchini Uingerea, huku mauzo ya tiketi kwa mashabiki wa kimataifa yakizinduliwa September 12.