Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo kati ya Marais wa Ukraine na Urusi yamtia moyo Ban

Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@UM

Mazungumzo kati ya Marais wa Ukraine na Urusi yamtia moyo Ban

Katibu Mkuu Wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameridhishwa na majadiliano kati ya Rais Vladmir Putin wa Urusi na Petro Poroshenko wa Ukraine huku akirejelea wito wake ya awali kwamba mazungumzo ya moja kwa moja ndio njia ya pekee ya kutatua mgogoro huo.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa japo maelezo ya kina kuhusu mazungumzo hayo hayakutolewa, Katibu Mkuu amepongeza mawasiliano kati ya viongozi hao.

Ban amesisitiza kwamba mpango kama huo unaweza tu kufanikiwa kama pande zote zitaonyesha nia njema na kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na mashauriano kati ya kundi la mataifa matatu pamoja na makundi ya waasi utakaofanyika ijumaa mjini Minsk.

Katibu Mkuu ameelezea imani yake kuwa Urusi itatumia uwezo wake kuyashawishi makundi yaliyojihami kukubali njia ya amani kama njia pekee ya utatuzi wa mgogoru huo wa Ukraine.