Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea haja ya juhudi za pamoja kukabiliana na tishio la Boko Haram

Said Djinnit.Picha ya UN

Ban aelezea haja ya juhudi za pamoja kukabiliana na tishio la Boko Haram

Ukiukwaji wa haki za binadamu utokanao na kuzorota hali ya usalama kaskazini mashariki mwaNigeriaunatia shaka, huku hali ya kibinadamu ikiwa imedhoofika mno, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. Ban amesema hayo katika ujumbe wake kwa mkutano wa tatu wa ngazi ya juu wa mawaziri kuhusu usalama nchiniNigeria, ambao umefanyika mjiniAbujaleo Septemba 3, akitaja haja ya umoja ili kukabiliana na hali hiyo.

Kwenye ujumbe huo uliosomwa na Mwakilishi wake wa ngazi ya juu nchini humo, Said Djinit, Ban amesema mkutano huo unaashiria kujitoa kwa mshikamano kwa jamii ya kimataifa kuunga mkono juhudi zaNigeriana ukanda wa Afrika ya Magharibi kukabiliana na tishio la Boko Haram.

Katibu Mkuu amesema bado anasikitishwa na kuendelea kwa ukatili kaskazini mashariki mwa nchi, ukiwemo mauaji ya raia wasio na hatia na utekaji wa wasichana, wanawake na wanaume. Ban amesema hali mbaya ya kibinadamu imeendelea kudhoofishwa na udhaifu wa wananchi kwa ujumla, kwani shule na shughuli za ukulima zimekatizwa, huku usalama wa chakula ukiwa unazorota zaidi.