Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yaanza tena safari za ndege kwenda Bentiu, Sudan Kusini

Picha: UNMISS

UM yaanza tena safari za ndege kwenda Bentiu, Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umeanza tena kufanya safari za ndege kwenda kwenye mji wa Bentiu, jimbo la Unity nchini Sudan Kusini.

Safari zote za ndege za abiria na mizigo zilikuwa zimesitishwa kufuatia kutunguliwa kwa ndege ya aina ya helikopta, iliyokuwa imekodeshwa kutumiwa mahsusi kwa shughuli za Umoja wa Mataifa wiki iliyopita.

Kaimu msemaji wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Joseph Contreras amesema kuwa safari za ndege sasa zinaendeshwakamakawaida. Amesema, kuwa mtaalam amewasili nchini humo kusaidia uendeshaji wa uchunguzi katika tukio la kutunguliwa kwa ndege wiki iliyopita.

(SAUTI YA CONTRERAS)

"Tulisitisha safari zetu za ndege baada ya kudunguliwa kwa helikopta ya UNMISS Agosti 26 karibu na Bentiu, lakini hata hivyo, siku ya Jumapili tulirejesha safari za ndege na ya kwanza  ilisafiri kutoka Malakal hadi uwanja wa ndege ulioko  Rubkonan Kaskazini mwa Bentiu".