Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa sheria ya kimataifa unakumbwa na changamoto- Afisa wa UM

UN Photo.
Serge Brammertz. Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimbari katika ilokuwa Jamhuri ya Yugoslavia (ICTY), Picha:

Mfumo wa sheria ya kimataifa unakumbwa na changamoto- Afisa wa UM

Mfumo wa sheria ya kimataifa kuhusu uhalifu unakumbwa na changamoto, kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimbari katika ilokuwa Jamhuri ya Yugoslavia (ICTY), Serge Brammertz.

Serge Brammertz amesema hayo baada ya kuhudhuria mkutano wa waendesha mashtaka wa kimataifa uliofanyika kwenye taasisi ya Robert Jackson karibu na mji wa Buffalo, Marekani hivi karibuni.

Mkutano huo ulihudhuriwa na waendesha mashtaka wa Mahakama kuhusu uhalifu wa kimbari Rwanda, Cambodia na Sierra Leone, pamoja na Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa, ICC.

Katika mahojiano na Derrick Mbatha wa Redio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Brammertz ameelezea zaidi kuhusu changamoto mfumo wa sheria ya kimataifa unazokumbana nazo.

(Sauti ya Brammertz)

"Kama mwendesha mashtaka wa kimatifa unafanya asilimia 100 ya kazi nje ya nchi, mfumo wa sheria siyo bayana, mara nyingi umma hawatoi ushirikiano  kwa sababu baadhi ya watu tunaowashtaki wanachukuliwa kama mashujaa katika jamii na mamlaka za kisiasi hawatoi ushirikiano vile vile  kwa sababu mara nyingi ndio watuhumiwa kwa hivyo inakuwa ngumu. Suala la kuwakamata watuhumiwa  ni changamoto kubwa kwa mahakama za kimataifa kwani tuna uwezo wa kukusanya ushahidi, kuuwasilisha kwa majaji lakini hatuna idara ya polisi ya kuwakamata washukiwa"