Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zanzibar yajizatiti kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Zanzibar yajizatiti kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Mkutano unaongazia maendeleo ya nchi za visiwa vidogo zinazoendelea (SIDS) ukiwa unachukua kasi nchini Samoa miongoni mwa nchi zinazowakilishwa humo ni Tanzania- Zanzibar, eneo ambalo limeshuhudia mabadiliko kadhaa  ya tabia nchi.

Ili kufahamu ni kwa kiwango gani nchi hiyo imeathiriwa na hatua zinazochukuliwa,  Daniel Dicknson wa Radio ya Umoja wa Mataifa aliyepiga kambi nchini Samoa amefanya mahojiano maalum na Waziri wa nchi ya ofisi ya makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, anayehusika na mazingira Fatma Fereji na kwanza ameanza kwa kumuuliza athari halisi za mabadiliko ya tabia nchi visiwani humo .

(SAUTI MAHOJIANO)