Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa nchi hawashughulikii maswala ya hali ya hewa kama inavyohitajika

Mary Robinson.Picha@UM

Viongozi wa nchi hawashughulikii maswala ya hali ya hewa kama inavyohitajika

Viongozi wa mataifa kote ulimwenguni hawashughulikii suala la hali ya hewa kikamilifu, hii ni kulingana na Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Mary Robinson.

Bi Robinson ameyasema hayo wakati mkutano wa tatu wa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea, SIDS ukiendelea Samoa.

Zaidi ya viongozi 125 wanatarajiwa kukutana katika kongamano kuhusu hali ya hewa mjini New York mwishoni mwa Septemba kwa ajili ya kuchagiza juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mratibu maalum Mary Robinson amesema kuwaleta pamoja viongozi hao wengi kutaleta mabadiliko.

Ni muhimu sana kwa sababu viongozi wa Mataifa hawajazungumizia suala la hali ya hewa vilivyo. waziri wao wa mazingira na wa kawi wamekuwa na maelngo. Lakini iwapo marais watakuwa na lengo itakuwa suala la wote. Ni suala la maendelao, ni suala la kifedha, ni suala la maadili, ni suala la kisiasa, ni suala la hayo yote."

Mataifa ya SIDS yanaathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo kuongezeka kwa maji baharini na viwango vya joto.