Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia bado iko na kitisho cha ukosefu wa chakula: Ripoti

Mvulana huyu akilinda ngamia katika soko la mifugo la Hergeisa kituo kilichofadhiliwa na FAO na fedha kutoka Uingereza.Picha@FAO

Somalia bado iko na kitisho cha ukosefu wa chakula: Ripoti

Zaidi ya watu milioni moja nchini Somalia wapo hatarini kukumbwa na tatizo la ukosefu wa chakula hatua ambayo itaongeza hali ngumu kwa taifa hilo ambalo katika miaka ya hivi karibuni limeshuhudia majanga kadhaa ikiwamo kujitokeza kwa hali ya ukame.

Ripoti iliyotolewa na mashirika ya kimataifa ikiwemo lile la chakula duniani, FAO inaonyesha kuwa idadi hiyo inajumuisha watoto zaidi ya 43,000 wanaokabiliwa na tatizo la utapiamlo.

Pia ripoti hiyo imebaini kuwepo kwa idadi ndogo ya misaada ya kibinadamu inayowafikia wananchi wa Somalia jambo ambalo linazorotesha ustawi wa kijamii.

Philippe Lazzarini ni mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Somalia anasema wengi wanaohitaji misaada wako maeneo ya ndani zaidi ambayo ni magumu kufikika lakini wanajaribu kufikisha misaada.

(Sauti ya Philippe)

 Jambo ambalo hatuwezi kufanya ni kuwapatia kiwango kikubwa cha misaada ya chakula hususan kwenye maeneo ya ndani zaidi.”

Kadhalika ripoti imesema kuwa sehemu kubwa ya taifa hilo linakabiliwa na ukosefu wa ajira na fursa za kimaendeleo ambazo zimetokana na kukosekana kwa biashara maalumu miongoni mwa jamii.