Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima Zanzibar ni mashuhuda wa athari za mabadiliko ya tabianchi

Picha:FAO(UN News Centre)

Wakulima Zanzibar ni mashuhuda wa athari za mabadiliko ya tabianchi

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, anayehusika na mazingira Fatma Fereji amesema athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa visiwa hivyo ni dhahiri akitaja jinsi ongezeko la kiwango cha maji ya bahari kinavyoharibu mazao ya wakulima.

Bi. Fereji amesema hayo alipohojiwa na Daniel Dicknson wa Radio ya Umoja wa Mataifa huko Samoa kando mwa mkutano wa tatu wa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea, SIDS.

(Sauti ya Fereji)

Waziri Fereji amesema matumaini kutoka mkutano huo ni kuanzisha ubia na wadau mbali mbali ili kuimarisha uwezo wao kwenye kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo kujenga uwezo wa wataalamu wao na hata kuwa na teknolojia za kisasa.