Harakati za kukabiliana na Ebola zaendelea
Ebola! Ebola! Ebola! Ugonjwa uliotikisa eneo la Afrika Magharibi kuanzia mwezi Machi mwaka huu ukijikita katika nchi Guinea, Liberia, Sierra Leone na hivi karibuni Nigeria. Hadi sasa watu zaidi ya 1500 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Shirika la Afya duniani kwa kuona dharura itokanayo na ugonjwa huo ilichukua uamuzi wa haraka wa kuruhusu matumizi ya dawa ambayo bado haijafanyiwa majaribio ili itumike kutibu wagonjwa wa Ebola. Hiyo ilikuwa ni moja tu ya hatua zilizochukuliwa kando ya nyingine nyingi. Je ni zipi hizo? Na wananchi wanachukulia vipi hatua hiyo? Basi ungana na Joseph Msami kwenye makala hii kuhusu Ebola!