Ujumbe kuhusu mabadiliko ya tabianchi sasa unafikia viongozi duniani:Ashe

1 Septemba 2014

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe amesema ujumbe kuhusu umuhimu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi sasa unafikia viongozi mbali mbali duniani

Amesema hayo kwenye mkutano wa Tatu wa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea, SIDS, mkutano unaofanyika huko Apia, Samoa, mkutano unaohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 100.

(Sauti ya Ashe)

 "Ni wazi kuwa kwa suala la mabadiliko ya tabianchi ambalo pengine ni kipaumbele cha SIDS, sauti sasa zimeanza kusikika na nchi za SIDS ziko makini sana kuhakikisha zinaweka bayana ajenda yao.”

 Ashe akizungumza kwenye mjadala kuhusu SIDS na maendeleo endelevu kwa wote, amesema ni vyema kutumia fursa ya sasa kuhakikisha kuwa ajenda ya maendeleo endelevu inakuwa na mantiki pia kwa nchi hizo za visiwa vidogo.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter