Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea SIDS, ripoti yaonyesha kuongezeka umaskini ukanda wa Pasifiki

Moja ya maeneo ya vijijini huko Samoa. (Picha:UNDP/ Abril Esquivel)

Kuelekea SIDS, ripoti yaonyesha kuongezeka umaskini ukanda wa Pasifiki

Ripoti ya shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP inaonyesha kuwa umaskini na hali ya kutokuwa na usawa vimeongezeka katika ukanda wa Pasifiki.

Ripoti hiyo inayoangazia hali ya maendeleo ya watu katika ukanda huo inaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya wanne katika visiwa kumi na mbili vilivyoko bahari ya Pasifiki wanaishi chini ya kiwango cha kimataifa cha umaskini.

Matokeo ya utafiti huu yametolewa wakati huu ambapo mkutano wa nchi zinazoendelea za visiwa vidogo, SIDS ukianza tarehe Mosi Septemba nchini Samoa.

Haoliang Xu  ni mkurugenzi wa  UNDP  Ukanda wa Asia na Pasifiki kuhusu umaskini.

(Sauti ya Xu)

"Nafikiri kuna sababu nyingi za kuongezeka kwa umaskini. Ripoti inasema kuwa kuna mabadiliko ya kimsingi katika jamii za ukanda huu. Nchi zinaathiriwa na utandawazi.  Vijana wanatafuta kazi na uchumi unabadilika kutoka uchumi tegemezi kwenda kwenye uchumi unaotegemea soko."