Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndugu watumia uimbaji kufikia ulimwengu

Bahati sisters (Picha ya UNHCR)

Ndugu watumia uimbaji kufikia ulimwengu

Baada ya kuishi maisha ya ukimbizini kwa muda mrefu hatimaye maisha yamebadilika. Ni maisha ya wasichana wanne ambao sasa wako ughaibuni nchini Canada lakini asili yao ni Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC nchi ambayo kwa muda mrefu imeshuhudia migogoro.Ungana na Priscilla Lecomte katika makala ifuatayo inayoeleza mkasa huu wa ndugu ambao wana ndoto za kuufikia ulimwengu na ambao msaada kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi umeweka nuru kwenye maisha yao.