Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya chanjo dhidi ya Surua nchini Burundi

Mtoto akipewa chanjo. Photo © UNICEF Burundi/Krzysiek

Kampeni ya chanjo dhidi ya Surua nchini Burundi

Lengo namba nne la maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa ni kupunguza kwa theluthi mbili vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ifikapo mwaka 2015.

Kufikia lengo hilo pamoja na mambo mengine nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinachukua hatua kadhaa ikiwemo kuwapatia watoto wachanga chanjo dhidi ya maradhi.

Mojawapo ya nchi hizo ni Burundi ambayo kwa ushirikiano na Shirika la Afya duniani WHO   wameanzisha wiki ya kampeni ya chanjo ya ziada kwa watoto dhidi ya maradhi ya Surua. Chanjo hiyo mpya ya ziada inatolewa mbali na chanjo ya kawaida ya miezi tisa.Hii imetokana na kuripotiwa kwa Surua katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Lengo ni kuutokomeza kabla ya mwaka wa 2020. Barani Afrika ni nchi 4 pekee zilizopata chanjo hiyo ya ziada dhidi ya Surua ikiwa ni pamoja na Ghana, Botswana, Sao Tome na Principe pamoja na Burundi.

Kutaka kujua jinsi shughuli hiyo ilivofanyika Burundi, jiunge na Mwandishi wetu Ramadhani KIBUGA katika makala haya.