Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO kuzindua ripoti kuhusu hali ya watu kujiua.

Tarik Jasarevic, Msemaji wa WHO, Geneva. Picha: UNIFEED Capture.

WHO kuzindua ripoti kuhusu hali ya watu kujiua.

Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki ijayo litatoa ripoti yake kwa mara ya kwanza kuhusu mbinu za kuzuia watu kujiua ikihusisha utafiti uliofanyika kwa miaka 10 kutoka nchi mbali mbali duniani. Taarifa zadi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

WHO imesema kuwa kujiua kunashika nafasi ya pili kwa ukubwa katika vifo na inatokea pote duniani, na inaathiri watu wenye umri mbali mbali. Pia shirika hilo limesema idadi ya wanaojiua duniani ni ya watu wenye miaka 70 na zaidi, lakini ndani ya nchi zingine, ni kwa watu wenye umri mdogo kuanzia maiak 15 hadi 29.

Tarik Jasarevic, ni msemaji wa WHO Geneva,

" Zaidi ya watu 800,000 hufa kila mwaka kutokana na kujiua, karibu mtu mmoja kila sekunde 40. Asilimia 75 ya vifo hivyo hutokea katika nchi zenye kipato cha chini na kati. Dawa ya sumu ya wadudu, kujinyonga, na silaha ndio mbinu za kawaida ya kujiua duniani kote."

WHO inasema kujiua kunazuilika kwa kupunguza uapatikanaji wa njia na mbinu zinazotumika kujiua na kuzitaka serikali kuanzisha njia za uratibu na utekelezaji . Hivi sasa nchi 28 pekee zinajulikana kuwa na mkakati wa kitaifa wa kuzuia vifo hivi.