Mkutano wa Afya na tabianchi Geneva watoa nuru Afrika

29 Agosti 2014

Wakati mkutano wa siku tatu kuhusu namna ya kukabiliana na athari za kiafya zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ukifikia ukomo leo huko Geneva, Uswisi, nchi za Afrika zimeazimia kukabiliana na majanga ya asili kama vile mafuriko ambayo huchangia madhara ya kiafya na kiuchumi.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii balozi wa kudumu wa Tanzania katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Modest Mero amesema nchi za ukanda wa Afrika zimetumia fursa hiyo kujifunza na kuchukua hatua na kwamba kipaumbele ni..

(SAUTI MERO)

Halikadhalika Balozi Mero amesema licha ya kutenga fedha za kushughulikia majanga kama hayo lakini pia ni muhimu kubadili tabia.

(SAUTI MERO)

Mkutano huo ulioratibiwa na shirika la afya duniani, WHO, na wadau wengine umewaleta pamoja washiriki 300 kutoka serikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia na wataaalamu wa mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter