Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akiwa Bali arejelea msimamo wake kuhusu mzozo Ukraine

UN Photo/Evan Schneider
Katibu mkuu Ban akihutubia mkutano wa sita wa jumuiko la ustaarabu, Bali Indonesia. Picha:

Ban akiwa Bali arejelea msimamo wake kuhusu mzozo Ukraine

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye yuko ziarani barani Asia akihudhuria mkutano wa sita wa kimataifa wa jumuiko la ustaarabu amezungumza na waandishi wa habari na kurejelea msimamo wake wa kutaka kupatiwa suluhu kwa mzozo wa Ukraine kwa njia ya amani. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Bwana Ban amesema hofu yake kubwa ni kile kinachoendelea kwenye mpaka kati yaUkrainena Urusi na maeneo yanayozunguka eneo hilo.

"Hii imebakia kikwazo kikubwa katika kupunguza kuendelea kuzorota kwa usalama eneo hilo kwani inaripotiwa kuwa silaha nzito zinaendelea kuingizwa Ukraine kutokea Urusi bila vikwazo vyovyote. Kuna umuhimu wa kuhakikisha kuna mipaka salama kati ya nchi mbili hizo chini ya uthibiti wa jumuiya ya kimataifa kama ilivyoridhiwa kwenye mazungumzo ya Minsk. Halikadhalika ni muhimu kuwa uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba ufanyike nchini koteg Ukraine na kuwe na mfumo wa kuhakikisha wananchi wote wanahisi wanawakilishwa vyema kwenye serikali ya Kiev.”

Mapema Ban alizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa Sita wa kimataifa wa jumuiko la ustaarabu na kusema kuwa jumuiko hilo limeleta mabadiliko duniani.

Ametolea mfano nchini Kenya ambako amesema limeweza kushawishi vijana kujiepusha na vikundi vya kigaidi ilhali huko Mindanao, linashawishi waislamu na wakristu kujitolea kwa pamoja kwa shughuli za kijamii.