Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano Mashariki mwa Ukraine yamtia hofu Ban

UN Photo.
Stephane Dujarric.

Mapigano Mashariki mwa Ukraine yamtia hofu Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na ripoti ya kwamba mapigano mashariki mwa Ukraine yanaenea kusini mwa nchi hiyo, karibu na mpaka wa Bahari ya Azov na Urusi.

Amesema iwapo repoti hizo zitathibitishwa basi hii itakuwa ni alama ya kuongezeka kwa hatari katika mgogoro nchiniUkraine.

Ban amesema Jumuiya ya kimataifa haiwezi kuruhusu hali hiyo kuzorota zaidi wala kuruhusu vurugu na uharibifu uliofanyika mashariki mwaUkraine.

Stephane' Dujarric ambaye ni msemaji wa Katibu Mkuu akawaeleza waandishi wa habari msimamo wa Ban.

(Sauti ya Dujaric )

 "Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anazingatia mkutano rasmi wa kwanza kati ya Marais wa Ukraine na Urusi uliofanyika Minsk Agosti 26. Ametoa wito kwa mazungumzo hayo yaendelee kwa minajili ya kutafuta njia ya Amani yakutatua mgogoro huu. Ban amehimiza pande zote kuchangia kupatikan kwa Amani katika nji ya ambayo itaheshimu uhuru na mpaka wa Ukraine."

Wakati huo huo, Dujarric amezungumzia kitendo cha kuongezeka kwa mapigano yaliyoanza jana kati ya kundi lililojiami na kikosi cha Jeshi laSyriakwenye eneo lililotengwa la milima ya Golan.

Inaelezwa kuwa wakati wa mapigano hayo askari wa kulinda amani 43 kutoka kikosi cha Umoja wa Mataifa ya uangalizi wa usitishaji mapigano (UNDOF) walishikiliwa na kikundi cha waasi katika maeneo ya jirani Al Qunaytirah.