Kilio cha vijana ni lazima kisikilizwe: Ban

28 Agosti 2014

Huko Bali Indonesia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza mwishoni mwa tukio la jumuiko la ustaarabu kwa vijana na kusisitiza kuwa dhana ya kwamba vijana ni viongozi wa kesho imepitwa na wakati. Taarifa kamili na Abdullahi Boru.

(Taarifa yaAbdullahi)

Katika hotuba yake wakati wa Mkutano huo, Ban amesema vijana wana majukumu muhimu katika jamii na hivyo kusema anapowatazama anaona viongozi wa leo na si wa kesho.

Anasema ni kwa kutambua hilo ndio maana alimteua mjumbe wake maalum kwa masuala ya vijana na ambaye hivi sasa anatumia uwezo wake kuwasilisha tashwiswhi za vijana katika majukwaa husika.

Ban ametaja mambo muhimu ya vijana kushughulikiwa kuwa ni pamoja na ajira zenye staha, mazingira salama ya  kazi na haki za binadamu.

Naye Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ustaarabu Nassir Al-Nasser akaelezea umuhimu wa jumuikohilo.

(Sauti ya Nasser)

"Tunaona ghasia, mapigano yanaendelea maeneo mengi duniani. Haya yanatokea wakati dunia inaibuka kwenye mdororo wa kiuchumi na sasa tunakumbana na mzozo wa kisiasa. Ukiangalia hapa na pale iwe ni mzozo wa kidini, kitamaduni au tofauti za rangi. Nafikiri ujumbe uko bayana hususan kutoka nchi kama Indonesia, nadhani utakuwa muhimu sana.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter