Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yazindua mpango wa kukabiliana na Ebola

Harakati za kujikinga dhidi ya Ebola. (Picha@WHO)

WHO yazindua mpango wa kukabiliana na Ebola

Shirika la afya duniani, WHO limezindua mpango wenye thamani ya karibu dola Milioni 490 utakaotoa mwongozo na kuratibu harakati za kimataifa dhidi ya mlipuko wa Ebola huko Afrika Magharibi. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Lengo la mpango huo ni kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo ndani ya miezi Sita hadi Tisa wakati huu ambapo umeshasababisha vifo vya watu 1552 kati ya wagonjwa 3069 hukoLiberia, Guinea, Sierra Leone na Nigeria.

WHO inasema asilimia 40 ya wagonjwa hao wamegundulika ndani ya wiki tatu na visa vimejikita katika maeneo machache lakini mpango utahusisha nchi zenye maambukizi na zile zilizo kwenye harakati za kudhibiti maambukizi.

Mathalani unataka nchi zipatiwe msaada kuondokana na vikwazo katika kudhibiti Ebolakamavile upatikanaji wa wahudumu wa afya, vifaa vya kujikinga na dawa za kuepusha maambukizi.

Dkt. Bruce Aylward ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO akihusika na operesheni za dharura anaelezea matumizi ya mpango huo.

(Sauti ya Dkt. Bruce)

 "Mpango utatumika kama muundo wa kutoa taarifa kila wakati kuhusumipango ya kina ya kazi. Kipaumbele kinaelekezwa kwenye mahitaji ya matibabu na vituo vya usimamizi, uhamasishaji wa kijamii, kuhakikisha mazishi ya waliokufa kwa Ebola yanafanyika salama. Mipango hii itatokana na taarifa halisi za eneo husika ambzo zinaanza kukusanywa wiki hii."