Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yazindua kampeni ya kupinga ndoa za utotoni Tanzania

Picha@UNFPA

UNFPA yazindua kampeni ya kupinga ndoa za utotoni Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu kwa kushirikiana na mfuko wa Graca Machel limezindua kampeni ya kupinga ndoa za utotoni nchini Tanzania.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii afisa wa UNFPA Sawiche Wamunza amesema kampeni hii inaenda sambamba na msukumo kwa serikali kubadilisha sheria ya kandamizi ya ndoa.

 (SAUTI SAWICHE)

Bi Wamunza amesema katika kufanikisha kampeni hii itakayoanzia mkoani Mara uliokithiri kwa ndoa za utotoni, viongozi wa dini na mila watahusishwa ili kufanikisha lengo.

 Kampeni hii endelevu inakuja wakati ambapo takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 41 duniani zenye idadi kubwa ya watoto wa kike wanaoozwa katika umri mdogo ambapo kwa wastani wasichana wawili kati ya watano wameolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.