Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya binadamu ina uhusiano na mabadiliko ya tabianchi:Ban

UN Photo/John Isaac
UN Photo/John Isaac

Afya ya binadamu ina uhusiano na mabadiliko ya tabianchi:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema hivi sasa ni dhahiri kuwa magonjwa yanayokumba binadamu yana uhusiano mkubwa na mabadiliko ya tabianchi yanayoendelea kutokea.

Ban amesema hayo katika ujumbe wake aliotoa kwa njia ya video kwenye mkutano wa shirika la afya duniani, WHO unaofanyika huko Geneva, Uswisi kuhusu afya na hali ya hewa, ukiwa ni wa kwanza wa aina yake.

(Sauti ya Ban)

Mkutano huo ulioandaliwa na unaangazia manufaa ya kiafya yasiyotambuliwa ambayo yanaweza kupatikana kwa kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumzia uhusiano huo, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan amesema kuna ushahidi wa kutosha mabadiliko ya hali ya hali ya hewa yanahatarisha afya ya wanadamu na kwamba suluhu zipo na hivyo ni lazima kubadilisha mwelekeo.