Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa DPI na asasi za kiraia wamulika maendeleo baada ya 2015

Picha@UN:DPI/NGO

Mkutano wa DPI na asasi za kiraia wamulika maendeleo baada ya 2015

"Hii ni fursa inayotokea mara moja kwa kizazi", amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, kwenye ujumbe wa video wakati wa uziduzi wa mkutano baina ya asasi za kiraia, NGOs na idara ya mawasiliano ya Umoja wa Mataifa, DPI.

Katika ujumbe huo Ban ameziomba asasi za kiraia zichukue fursa hiyo kujenga dunia bora zaidi kwa ajili ya vizazi vijavyo akisema:

(sauti ya Ban)

“ Malengo ya maendeleo ya milenia yamefanikiwa kuleta mabadiliko , kwa kuondoa umaskini miongoni mwa watu wengi, kurejesha watoto wengi zaidi shuleni, na kuzuia magonjwa mengine zaidi. Nawashukuru kwa kuchangia katika mafanikio haya. Pia nawaomba muongeze bidii”

Kwa upande wake Samantha Power ambaye ni mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa amesema amefurahi kuona mashirika mengi yanakutana kwa ajili ya kupambana na umaskini, akisisitiza eneo moja:

(Sauti ya Samantha)

Tunahitaji kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Ni bahati kwamba leo tunaelewa tusipopambana na mabadiliko ya tabianchi kwa uthabiti,  matokeo yake mabaya yataondosha kabisa mafanikio tunayojaribu kupata kwa upande mwingine. Mabadiliko ya tabianchi pia yanatufundisha kwamba hatuwezi kuandaa malengo kwa ajili ya sehemu moja tu ya dunia. Matokeo yetu mapya yanapaswa kufaa kila nchi, jinsi yanapaswa kuundwa na kila nchi”